MWENYEKITI TSC APONGEZA HUDUMA ZITOLEWAZO KATIKA MAONESHO YA SIKU YA MWALIMU DUNIANI

18 Nov, 2026
MWENYEKITI TSC APONGEZA HUDUMA ZITOLEWAZO KATIKA MAONESHO YA SIKU YA MWALIMU DUNIANI

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Prof. Masoud Hadi Muruke, amefanya ziara katika mabanda ya maonesho yanayofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square, Dodoma, na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi na wadau katika kuadhimisha Siku ya Mwalimu Duniani.

Prof. Muruke alifanya ziara hiyo leo, Oktoba 1, 2026, akiwa ameambatana na Katibu wa Tume, Mwl. Paulina M. Nkwama, ambapo alitembelea mabanda mbalimbali na kupata maelezo kuhusu huduma, taarifa na elimu inayotolewa kwa wananchi na wadau.

Maonesho hayo yaliyoandaliwa na TSC yanafanyika kuanzia tarehe 1 hadi 5 Oktoba 2026 katika Viwanja vya Nyerere Square, Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani, sambamba na kuadhimisha miaka 10 ya Tume tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumza baada ya kutembelea mabanda hayo, Prof. Muruke amepongeza juhudi zinazofanywa na TSC pamoja na taasisi na wadau wanaoshiriki katika maonesho hayo kwa kuhakikisha huduma na taarifa muhimu zinawafikia wananchi kwa urahisi.

Amesisitiza umuhimu wa taasisi za umma kutumia maonesho na majukwaa kama hayo kuwafikia wananchi moja kwa moja, kutoa elimu kuhusu huduma zinazotolewa na kupokea mrejesho wa wananchi kwa lengo la kuendelea kuboresha utoaji wa huduma.

Katika maonesho hayo, TSC inashirikiana na taasisi na wadau mbalimbali, wakiwemo Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Watumishi Housing Investment (WHI), Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Benki ya NMB.

Mbali na huduma na elimu inayotolewa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu walimu na wananchi kwa ujumla, maonesho hayo pia yamekuwa na huduma ya uchangiaji damu inayotolewa na Wakala wa Damu Salama, ambapo wananchi wanahamasishwa kujitokeza kuchangia damu na hivyo kusaidia kuokoa maisha ya wenye uhitaji.

Maonesho hayo yanaendelea hadi Oktoba 5, 2026, huku TSC ikiwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali kufika katika Viwanja vya Nyerere Square, Dodoma, kupata huduma, taarifa na elimu kuhusu shughuli na huduma zinazotolewa na Tume pamoja na taasisi washiriki.

slot gacor