Kupandisha cheo Walimu

UPANDISHAJI VYEO WALIMU

Kanuni Na. 8 ya Kanuni za Utumishi wa Walimu za Mwaka 2016 imefafanua sifa zinazotakiwa ili mwalimu aweze kupandishwa cheo. Aidha, Waraka Na. 1 wa Mwaka 2014 uliotolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, unaohusu utaratibu wa kupandisha cheo Watumishi wa Umma wakiwemo Walimu umeelekeza utaratibu wa kuzingatiwa katika kupandisha cheo. Mambo muhimu ya kuzingatiwa ni pamoja na: -

  1. Uwepo wa Muundo wa Kada ya Mwalimu;
  2. Uwepo wa Tange iliyohuishwa;
  3. Uwepo wa Bajeti ya mishahara na Ikama iliyoidhinishwa;
  4. Mwalimu anayepandishwa cheo lazima awe amethibitishwa kazini;
  5. Hatakiwi kuwa na tuhuma yoyote ya kinidhamu;
  6. Awe na utendaji kazi mzuri uliopimwa katika Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu; na
  7. Awe na uzoefu wa kutosha katika cheo anachokitumikia kwa kadri maelekezo yatavyotolewa na Serikali