TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA NA ELIMU

14 Apr, 2023

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

        TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

 

 

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA NA ELIMU

 

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imepata kibali cha ajira za Watumishi wa Kada za Afya 8,070 kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati pamoja na Ualimu 13,130 wa Shule za Msingi na Sekondari watakaofanya kazi chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

 

Hivyo, wahitimu kutoka kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kuanzia tarehe 12 - 25 Aprili, 2023. Nafasi za ajira zilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada (Degree).

 

A: TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA ZA UALIMU

Waombaji wote wenye sifa watume maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz. Tangazo hili linawahusu wahitimu wa Kozi za Ualimu kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2022. Waombaji waliowahi kutuma maombi yao awali kupitia mfumo wa maombi ya ajira wanatakiwa kuhuisha taaarifa zao kwenye mfumo.

 

1.0         SIFA ZA WAOMBAJI

1.1    SIFA ZA KITAALUMA ZA MWOMBAJI

Walimu wanaotakiwa kutuma maombi wawe na sifa za kitaaluma kama ifuatavyo:

1

 

 

 

1.2    WALIMU WA SHULE ZA MSINGI

 1. Mwalimu Daraja la III A - Mwenye Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi, Elimu ya Michezo, Elimu Maalum na Elimu ya Awali (certificate in primary education);
 2. Mwalimu Daraja la IIIB- Awe na stashahada ya ualimu (diploma) waliosomea elimu ya Msingi.
 3. Mwalimu Daraja la IIIC- Awe na shahada ya Ualimu kwa Elimu ya Awali.

 

1.3    WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI

i. Mwalimu Daraja la III B – Awe mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu aliyesomea Elimu Maalum kwa masomo ya English Language, Literature in

English, Biology, Chemistry, Physics na Mathematics; ii. Mwalimu Daraja la III C – Awe mwenye Shahada ya Ualimu aliyesomea Elimu Maalum kwa  masomo  ya  English  Language, Literature in English, Biology,

Chemistry, Physics na Mathematics; iii. Mwalimu Daraja la III B - Awe mwenye Stashahada ya Ualimu wa somo la English Language, Literature in English, Biology, Chemistry, Physics na Basic

Mathematics; iv. Mwalimu Daraja la III C – Awe mwenye Shahada ya Ualimu wa somo la English Language, Literature in English, Biology, Chemistry, Physics na Basic

Mathematics;

v. Fundi Sanifu wa Maabara – Awe na Stashahada ya Ufundi Sanifu Maabara au Stashahada ya Sayansi na Teknolojia ya Maabara.

2

 

B. TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA KADA ZA AFYA

 

Wataalamu wa Kada za Afya wenye sifa wanatakiwa kufuata utaratibu ule ule wa  kutuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz. Waombaji ambao waliowahi kutuma maombi yao awali kupitia mfumo huu wanatakiwa kuhuisha taarifa zao.

 

2.0  Sifa za Kitaaluma za Waombaji wa Kada za Afya

2.1 Daktari Bingwa Daraja la II  – TGHS G  

Waombaji wanatakiwa kuwa na,

 1. Shahada ya Uzamili ya Udaktari wa Binadamu au Phd ya udaktari wa binadamu ya miaka mitatu au zaidi kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na wawe wamemaliza mafunzo ya kazi “Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja;
 2. Usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of

Tanganyika); na iii. Leseni hai kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

 

2.2  Daktari Daraja la II  – TGHS E  Waombaji wanatakiwa kuwa na,

 1. Shahada ya udaktari wa binadamu kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na wawe wamemaliza mafunzo ya kazi “Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja;
 2. Usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika); na
 3. Leseni hai kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

 

 

 

 

2.3  Daktari wa Meno Daraja la II  – TGHS E  

Waombaji wanatakiwa kuwa na,

 1. Shahada ya udaktari wa Meno kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na

Serikali na wawe wamemaliza mafunzo ya kazi “Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja;

 1. Usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of

Tanganyika); na

 1. Leseni hai kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

 

2.5 Daktari Msaidizi Daraja la II  – TGHS C  

Waombaji wanatakiwa kuwa na,

 1. Stashahada ya juu ya udaktari kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na wawe wana uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu;
 2. Usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of

Tanganyika); na

 1. Leseni hai kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

 

2.6 Daktari wa Meno Msaidizi Daraja la II  – TGHS C  

Waombaji wanatakiwa kuwa na,

(iv) Stashahada ya udaktari wa Meno kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na wawe wana uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu;

 1. Usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of

Tanganyika); na

 1. Leseni hai kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

 

 

2.7  Tabibu Meno Daraja la II - TGHS B 

Waombaji wanatakuwa kuwa na,

 1. Stashahada ya Tabibu Meno (Diploma in Clinical Dentistry/NTA level 6) ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali;
 2. Usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of

Tanganyika); na iii. Leseni hai kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

 

2.8 Tabibu Daraja la II - TGHS B  Waombaji wanatakiwa kuwa na,

 1. Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine) ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali; na
 2. Leseni hai kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

 

2.9  Tabibu Msaidizi - TGHS A  Waombaji wanatakiwa kuwa na,

i.      Astashahada ya miaka miwili ya Tabibu Wasaidizi (Clinical Assistant Certificate

NTA level 5)  kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali; na ii. Leseni hai kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

 

2.10 Mteknolojia (macho) Daraja la II TGHS – B 

Waombaji wanatakiwa wawe Wahitimu wa Stashahada katika fani ya Uteknolojia ya muda wa miaka mitatu katika fani ya Macho kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Mabaraza pale inapohusika.

 

 

 

2.11 Mteknolojia (Mionzi) Daraja la II TGHS – B

Waombaji wanatakiwa kuwa na, 

 1. Stashahada katika fani ya Mionzi (Diploma in Radiology/Radiography/NTA leve 6) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali;
 2. Usajili kutoka Baraza la Wataalamu wa Mionzi Tanzania (The Medical Radiology and

Imaging Professionals Council); na iii. Leseni hai kutoka Baraza la Wataalamu wa Mionzi Tanzania (The Medical Radiology and Imaging Professionals Council).

 

2.12 Mteknolojia (Dawa) Daraja la II TGHS – B

Waombaji wanatakiwa wawe Wahitimu wa Stashahada katika fani ya Uteknolojia ya muda wa miaka mitatu katika fani ya Dawa kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wafamasia.

 

2.13 Mteknolojia (Meno) Daraja la II TGHS – B

 Waombaji wanatakiwa wawe Wahitimu wa Stashahada katika fani ya Uteknolojia ya muda wa miaka mitatu katika fani ya Meno kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari Tanganyika.

 

2.14 Mteknolojia (Maabara) Daraja la II TGHS – B

Waombaji wanatakiwa wawe Wahitimu wa Stashahada katika fani ya Uteknolojia ya muda wa miaka mitatu katika fani ya Maabara kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara (Health

Laboratory Practitioners’ Council).

 

2.15 Afisa Muuguzi Daraja la II TGHS – C 

Waombaji wanatakiwa kuwa na,

 1. Shahada ya Uuguzi kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu mafunzo kwa vitendo (Internship) ya mwaka mmoja;

 

 1. Awe amesajiliwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and

Midwifery Council); na iii. Leseni hai kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council)

 

2.16 Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II TGHS – B  

Waombaji wanatakiwa kuwa na,

i. Stashahada ya Uuguzi (Diploma) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and

Midwifery Council); na ii. Leseni hai kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council).

 

2.17 Muuguzi Daraja la II TGHS – A 

Waombaji wanatakiwa kuwa na,

i. Astashahada (cheti) ya miaka miwili ya Uuguzi na Ukunga (Certificate in Nursing and Midwifery/NTA leve 5) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa

(Enrolled) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania,  ii. Leseni hai kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council).

 

2.18 Mfamasia Daraja la II - TGHS D

Waombaji wote wanatakiwa kuwa na,

 1. Waombaji wawe na Shahada ya Famasi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na waliohitimu mafunzo kwa vitendo (Internship) ya mwaka mmoja na ambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi (Pharmacy Council); 
 2. Wawe na  Leseni hai kutoka Baraza la Wafamasia Tanzania.

 

 

 

2.19 Fundi Sanifu Msaidizi Vifaa Tiba Daraja la II - TGHS A 

Waombaji wawe na Cheti cha Ufundi Daraja la II kutoka Chuo kinachotambuliwa na

Serikali.

 

2.20 Afisa Ustawi wa Jamii Daraja la II – TGS D

Waombaji wawe na Shahada au Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) katika mojawapo ya fani zifuatazo: Social Work, Sociology, Psychology, Social Protection, Guidance and Counceling, Theology, Divinity, Child Protection, Social Policy, Early Childhood Development, Social Gerontology, Dietetics au fani nyingine zinazofanana na Ustawi wa Jamii kutoka Chuo cha Elimu ya Juu kinachotambuliwa na Serikali.

 

2.21 Afisa Mteknolojia (Maabara) Daraja la II – TGHS C

Waombaji wawe na Shahada ya Sayansi ya Maabara ya Afya (Health Laboratory Scientists) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na

Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).

 

2.23 Afisa Fiziotherapia Daraja la II – TGHS C

Waombaji wawe na Shahada ya Fiziotherapia (Bachelor of Science in Physiotherapy) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. 

 

2.24 Fiziotherapia Daraja la II – TGHS B

Waombaji wawe Wahitimu wa Kidato cha nne/sita wenye Stashahada ya miaka mitatu (3) katika Fani ya Fiziotherapia/Mtoa tiba kwa Vitendo kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. 

 

2.25 Mteknolojia Msaidizi Maabara – TGHS A

Waombaji wawe na Astashahada katika fani ya Uteknolojia wa Maabara ya Afya (Certificate in Health Laboratory Science) kwa muda wa miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).

2.26 Mteknolojia Msaidizi Dawa – TGHS A

Waombaji wawe na Elimu ya Kidato cha nne wenye Astashahada katika fani ya Uteknolojia wa Dawa kwa muda wa miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wafamasia.

 

2.27 Mteknolojia Msaidizi Meno – TGHS A

Waombaji wawe na Elimu ya Kidato cha nne wenye Astashahada katika fani ya Uteknolojia wa Meno kwa muda wa miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari Tanganyika.

 

2.28 Mteknolojia Msaidizi Macho – TGHS A

Waombaji wawe na Elimu ya Kidato cha nne wenye Astashahada katika fani ya

Uteknolojia wa Macho kwa muda wa miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari Tanganyika

 

2.29 Katibu wa Afya  - TGHS C

Waombaji wawe na Shahada ya Uongozi wa Huduma za Afya (Health Services Administration) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.

 

2.30 Afisa Afya Mazingira Daraja II - TGHS C

Waombaji wawe na Shahada ya Sayansi za Afya ya Mazingira na mafunzo kazini kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa na Baraza la Wataalamu wa

Afya ya Mazingira (The Environmental Health Practitioners’ Registration Council).

 

2.31 Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja II – TGHS B

Waombaji wawe na Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira ya miaka mitatu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa na Baraza la Wataalamu wa

Afya ya Mazingira (The Environmental Health Practitioners’ Registration Council).

 

 

2.32 Msaidizi wa Afya (Mazingira) - TGHS A

Waombaji wawe wahitimu wa kidato cha nne wenye cheti cha miaka miwili cha mafunzo ya Msaidizi wa Afya au Fundi Sanifu Afya Mazingira kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Afya ya

Mazingira (The Environmental Health Practitioners’ Registration Council).

 

2.33 Afisa Lishe II – TGS D

Waombaji wawe na Shahada ya kwanza ya Lishe, Sayansi Kimu na Lishe au Sayansi ya Chakula na Teknolojia ya Chakula (BSc - Nutrition, Home Economics and Nutrition, Food Science and Technology, Food Science) au Stashahada ya Juu ya Lishe (Higher Diploma in Nutrition) kutoka Chuo cha Elimu ya Juu kinachotambuliwa na

Serikali.

 

2.34 Dobi II - TGHS B

Waombaji wawe na Elimu ya kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya miaka miwili au mitatu katika fani ya Dobi (Laundry Services) kutoka katika vyuo vinavyotambulika na Serikali.

 

2.35 Msaidizi wa Afya – TGHOS A

Waombaji wawe na Elimu ya kidato cha Nne waliofuzu mafunzo ya mwaka mmoja katika fani ya Afya, Afya Ngazi ya Jamii au Mafunzo yoyote yanayofanana na hayo kutoka Chuo cha Afya kinachotambuliwa na Serikali. 

 

3.0   MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI

Waombaji wote wanatakiwa kuwa na sifa za jumla kama ifuatavyo:

 1. Awe raia wa Tanzania;
 2. Awe na umri usiozidi miaka 45;
 3. Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha Kidato cha Nne, Sita, Taaluma na usajili kamili (Full Registration) au Leseni hai ya kufanya kazi ya taaluma husika);
 4. Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali;
 5. Waombaji walioajiriwa kwa mkataba wa ajira kutoka kwa Wadau wa Maendeleo katika Sekta ya Afya wanatakiwa kuambatisha nakala za mkataba na barua za uthibitisho kutoka kwa Wakurugenzi wa Halmashauri husika;
 6. Awe hajawahi kufukuzwa, kuacha kazi au kustaafishwa katika Utumishi wa Umma;
 7. Awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA); na 
 8. Aambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.

 

4.0   MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI WOTE

 1. Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi katika Halmashauri/Vituo

watakavyopangiwa;

 1. Waombaji wawe tayari kufanya kazi na Mashirika au Taasisi zilizoingia Ubia na

Serikali; iii. Baada ya kupangiwa  kituo  cha  kazi, hakutakuwa  na  nafasi  ya kubadilishiwa kituo cha kazi;

 1. Waombaji wote wahakikishe wanajaza taarifa zao na kuambatisha nyaraka zote muhimu kwenye mfumo; na
 2. Maombi ya ajira ni bure.

 

5.0   WAHITIMU WALIOSOMA NJE YA NCHI

 1. Waombaji wote waliosoma Elimu ya Sekondari nje ya nchi wanatakiwa kupata Namba ya Ulinganifu wa Matokeo (Equivalent Number) inayoanza na Herufi EQ… kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania ili kuwawezesha kuingia kwenye Mfumo wa

Ajira; na

 1. Waombaji waliosoma Vyuo vya Nje ya Nchi wanatakiwa kupata Ithibati ya masomo yao kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ili vyeti vyao viweze kutambuliwa na kupata uhalali wa kutumika hapa nchini.

 

 

Ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na sifa za waombaji na taratibu za utumaji wa maombi kwa nafasi za Kada za Afya na Elimu, tafadhali bofya: www.tamisemi.go.tz au wasiliana na Kituo cha huduma kwa wateja cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa namba za simu 026 2160210 au 0735 160210.

 

Waombaji wenye Ulemavu na sifa zilizoainishwa katika tangazo hili watume maombi yao pia kupitia mfumo. Aidha, maombi yao yaeleze aina ya ulemavu alionao na kuambatisha picha na uthibitisho wa daktari kutoka katika hospitali za Serikali na yatumwe katika anwani ifuatavyo:

 

  Maombi yoyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwa moja Ofisi ya Rais - TAMISEMI hayatafanyiwa kazi. Aidha, waombaji watambue kuwa ukishapangiwa kituo hauruhusiwi kuhama au kubadilisha kituo kwa muda wa miaka mitano.

 

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 25 Aprili, 2023 saa 05:59 usiku. Tangazo hili linapatikana katika tovuti ifuatayo: www.tamisemi.go.tz

 

Limetolewa na:    Katibu Mkuu,

Ofisi ya Rais - TAMISEMI, 

Mji wa Serikali - Mtumba,

S.L.P 1923,

41185 DODOMA.

 

 1. Aprili, 2023.