Kusimamia mpango wa mafunzo kwa Walimu

KUSIMAMIA MPANGO WA MAFUNZO

Kifungu cha (5) (g) cha Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu Na. 25 ya mwaka 2015 kimeipa Tume jukumu la kusimamia Mpango wa Mafunzo ya Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari. Mpango huu wa mafunzo huandaliwa na Mwajiri na kazi ya Tume ni kufuatilia utekelezaji wa mpango ulioandaliwa. Tume huhakikisha Mpango wa Mafunzo unaandaliwa kwa kuzingatia mahitaji ya mafunzo. Walimu wanapokwenda masomoni hata kama wapo kwenye Mpango wa Mafunzo wanapaswa pia kupewa ruhusa ya maandishi.