Msambao wa Walimu

KUHAKIKISHA UWIANO SAWA KATIKA USAMBAZAJI WA WALIMU NCHINI

Kifungu cha (5) (i) cha Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu Na.25 ya Mwaka 2015 kimeipa Tume jukumu la kusimamia na kuhakikisha kuwa kuna uwiano wa usambazaji wa Walimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Shule. Jukumu hili hutekelezwa na Tume kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

  1. Tume ngazi ya Wilaya itafuatilia kwa Waajiri kujua idadi ya Walimu katika kila Shule, mahitaji, upungufu na ziada na kumshauri Katibu wa Tume kuhusu hali ya Walimu kiwilaya na kishule;
  2. Katibu wa Tume atamshauri Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa kuhusu hali ya Walimu nchini (Idadi ya Walimu na upungufu uliopo kiwilaya na kishule);
  3. Wizara yenye dhamana na Serikali za Mitaa itaomba kibali cha ajira kwa Katibu Mkuu - UTUMISHI;
  4. Wizara yenye dhamana na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) itapokea orodha ya Walimu wenye sifa kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;
  5. Tume ya Utumishi wa Walimu kwa kushirikiana na TAMISEMI itahakiki orodha iliyowasilishwa, itafanya uchambuzi na kuwapanga Walimu wenye sifa kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa kulingana na mahitaji na nafasi zilizopo (Kibali cha ajira);
  6. Walimu wataripoti kwenye vituo walikopangiwa na kulipwa stahiki zinazoambatana na kuanza kazi.