Kuthibitisha kazini Walimu

KUTHIBITISHA KAZINI WALIMU

anuni ya 5 (1) – (5) ya Kanuni za Tume ya Utumishi wa Walimu za mwaka 2016 zimeelekeza utaratibu wa kuwathibitisha kazini Walimu. Utaratibu unaelekeza kuwathibitisha kazini walimu ambao wamemudu majukumu ya kazi au kusitisha ajira / kumwongezea muda wa majaribio Mwalimu ambaye ameshindwa kumudu vyema majukumu (hawajakidhi vigezo) baada ya kumaliza muda wa matazamio (Probationary Period) uliowekwa kisheria.

  1. Mwalimu anapaswa kuthibitishwa kazini ndani ya miezi 12 tangu alipoajiriwa kwa mara ya kwanza kwenye Utumishi wa Umma; Mkuu wa Shule atatoa taarifa ya Utendaji kazi wa Mwalimu katika kipindi cha Matazamio.
  2. Miezi mitatu kabla ya kumalizika kwa kipindi cha matazamio yaani (Miezi 12), Mamlaka ya Serikali za Mitaa husika itapeleka tathmini na mapendekezo ya Walimu waliokidhi vigezo kwenye Ofisi za Tume ngazi ya Wilaya;
  3. Tume ngazi ya Wilaya itachambua na kuwasilisha kwenye Kikao cha Kamati ya Wilaya mapendekezo ya walimu waliokidhi vigezo na ambao wanastahili kuthibitishwa kazini;
  4. Kamati ya Wilaya itatoa uamuzi iwapo walimu husika wathibitishwe kazini  au kipindi cha matazamio kiongezwe ili kumpa Mwalimu nafasi ya kujirekebisha au ajira yake isitishwe;
  5. Mwalimu atajulishwa kwa barua juu ya uamuzi uliofikiwa ikiwemo kuandikiwa barua ya kuthibitishwa kazini kwa waliokidhi vigezo. Iwapo Mwalimu atakuwa ameongezewa muda wa kipindi cha matazamio, muda huo haupaswi kuzidi miezi sita (6).