Kubadilisha cheo walimu waliojiendeleza kielimu

KUWABADILISHIA CHEO/KAZI  WALIMU WALIOJIENDELEZA KIELIMU

Kubadilisha cheo/kazi kupo kwa aina mbili; aina ya kwanza ni kumbadilisha cheo mtumishi kutoka muundo mmoja kwenda mwingine na jukumu hili linafanywa kwa kupata kibali maalum kutoka kwa Katibu Mkuu-UTUMISHI. Aina ya pili ni kumbadilisha mtumishi cheo kutoka cheo kimoja kwenda kingine. Kubadilisha kazi/cheo kunakofanywa na TSC ni kumbadilishia Mwalimu cheo kwenye kada ya ualimu. Walimu katika Utumishi wa Umma wamegawanyika katika kada/makundi makuu matatu kama yalivyoainishwa katika Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Na. 1 wa Mwaka 2014 kuhusu Miundo ya Utumishi wa Kada za Walimu chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambayo ni

  1. Walimu Daraja A – hawa ni Walimu wa ngazi ya Cheti;
  2. Walimu Daraja B – hawa ni Walimu wa ngazi ya Stashahada na;
  3. Walimu Daraja C – hawa ni Walimu wa ngazi ya Shahada.
  4. Ili Mwalimu aweze kubadilishiwa cheo/kazi mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:-
  5. Awe amehitimu na kufuzu mafunzo katika kada ya ualimu katika ngazi ya stashahada au shahada katika chuo kinachotambuliwa na Serikali;
  6. Awe na cheti halisi cha kuhitimu;
  7. Awe ametengewa Ikama na Bajeti ya mishahara kwa mwaka husika

 

TANBIHI: Kubadilisha cheo/kazi pia kunazingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali