Ajira na Usajili

AJIRA NA USAJILI WA WALIMU

Utaratibu wa ajira na usajili umeainishwa kwenye Kanuni Na. 3 (a) – (d) ya    

Kanuni za Tume ya Utumishi wa Walimu za Mwaka 2016. Utaratibu huo unahusisha Mwalimu, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC).

Utaratibu huu unaanza tangu Mwalimu anapoajiriwa na kupangiwa Kituo cha kazi hadi anaposajiliwa.  Walimu wanapokuwa wamepangiwa na kuripoti vituoni watalazimika kujaza mikataba ya ajira kwa masharti ya kudumu na Waajiri. TSC watahakiki Mikataba hiyo kwa kuhakikisha kuwa ina viambatisho muhimu vilivyoainishwa. Baada ya kukamika kwa zoezi la ujazaji wa Mkataba, Mwalimu atasajiliwa na kupewa namba ya usajili (TSC Na.) na Ofisi ya Tume ngazi ya Wilaya.