Bw. Gerard J. Chami

Gerard J. Chami photo
Bw. Gerard J. Chami
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

Barua pepe: gerald.chami@tsc.go.tz

Simu:

Wasifu

Ndg. Gerard Julius Chami,

MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI.

Ndg. Chami aliteuliwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali tarehe 21 Septemba, 2015. Chami ana uzoefu na weledi wa miaka 23 katika Masuala ya Mawasiliano ya Umma, Habari, Uhusiano wa Umma, Masoko na Matangazo, Usimamizi wa Ujasiriamali, Utawala katika Biashara, Ubunifu na Usanifu wa Machapisho, Uandaaji wa Picha Jongefu, Mawasiliano ya Kimkakati katika Dharura za Sekta ya Afya na Ushirikishwaji wa Jamii, Elimu kwa Umma, Mipango Shirikishi na Demokrasia, Usimamizi kwa Matokeo, Mapitio na Uchambuzi wa Mipango ya Bajeti kwa ajili ya Usimamizi wa Taasisi za Umma na Mashirika yaliyoanzishwa Kisheria, Upangaji Mkakati na Utekelezaji kwa Ufanisi, Usimamizi wa Hatari za Biashara, Usimamizi wa Mifuko ya Uwekezaji ya Umma, Kuandaa Uzalishaji wa Vipindi vya Kielektroniki vya Elimu kwa Umma, Sheria ya Manunuzi ya Umma, Kanuni na Zana za Utekelezaji wa Ununuzi, Mkakati wa Mawasiliano ya Kibiashara pamoja na Itifaki kwa ujumla wake akitumikia katika Utumishi wa Umma na Sekta Binafsi.

Kabla ya uteuzi wake, Ndg. Chami alikuwa akikaimu nafasi hiyo akiwa Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Kitengo cha Uhusiano wa Umma, Habari na Mawasiliano katika Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP).

Katika utumishi wake, Ndg. Chami ameshika nafasi na nyadhifa mbalimbali za usimamizi na uongozi katika maeneo tofauti yakiwemo; Ofisi ya Rais – Tume ya Utumishi wa Walimu (PO-TSC), Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (sasa Wizara ya Afya), Wizara ya Fedha na Mipango – Ofisi ya Msajili wa Hazina, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Shirika la Elimu Kibaha), Royal Public Relations and Productions (RPRP), Royal College of Tanzania (RCT), Upendo Fm Radio, Ukweli Fm Radio, Gazeti la Kiongozi, Nipashe, Alasiri, Majira, Dar Leo, Mwananchi na Runinga ya Taifa (TVT) sasa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC).

Hata hivyo, katika utumishi wake, Ndg. Chami amesimamia na kutekeleza majukumu kadhaa ya ziada akiwa; Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Ofisi ya Rais – Tume ya Utumishi wa Walimu (PO-TSC Sports Club), Mjumbe wa Kamati ya Mapitio ya Maudhui ya Zana na Vielelezo vya Uelimishaji Jamii na Uhamasishaji wa Masuala mbalimbali ya Afya chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (MoHCDGEC), Mweka Hazina Msaidizi - Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali Tanzania (TAGCO), Mjumbe wa Kamati ya Ushauri na Bodi ya Wakurugenzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar Es Salaam (DSJ), Mjumbe wa Kamati ya Ushauri wa Chuo cha Royal Tanzania (RCT), Mjumbe Mtendaji wa Jumuiya ya Huduma za Kujitolea Tanzania (TVSM) sasa (TAVODET), na Mwanachama hai wa Jumuiya ya Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino nchini Tanzania (SAUT).