DK. MSONDE AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SHULE YA MSINGI KIGURUNYEMBE, AINGIA MOJA KWA MOJA DARASANI

25 Apr, 2023
DK. MSONDE AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SHULE YA MSINGI KIGURUNYEMBE, AINGIA MOJA KWA MOJA DARASANI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Searikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Dkt. Charles Msonde tarehe 24 Aprili 2023 alifanya ziara ya kushtukiza katika shule ya Msingi Kigurunyembe iliyopo katika Manispaa ya Mkoa wa Morogoro ambapo alikwenda moja kwa moja darasani kujionea umahiri wa wanafunzi katika masomo wanayofundishwa.

 

Naibu Katibu Mkuu huyo alitembelea darasa la saba, la sita na la tatu ambapo katika madarasa hayo alitaka kuona umahiri wa wanafunzi hao katika kujieleza kwa lugha ya kiingereza.

 

Baada ya kuwahoji na kusikiliza namna wanafunzi hao wanavyojieleza, Dkt. Msonde alionesha kurudhishwa kiwango cha ujuzi wa wanafunzi hao huku akiwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na uzalendo huku akisema juhudi hizo zinaunga mkono jitihada za Serikali za kufanya maboresho katika sekta ya elimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata ujuzi na umahiri katika masomo yao.

 

“Kama tunavyoona walimu wetu wanafanya kazi kubwa, kumsimamia mwanafunzi wa darasa la tatu hadi kuwa na uwezo mzuri wa kujieleza namna hii siyo kazi ndogo. Na hii siyo kwa shule hii peke yake, ukienda shule yoyote ya msingi utaona namna walimu wanavyojitoa kufundisha wanafunzi. Hivyo, tunafarijika sana kuona walimu wetu wana mwitikio chanya katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha elimu,” alisema.

 

Pamoja na kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi na maarifa, Dkt. Msonde alisema walimu wana jukumu la malezi kwa watoto ambapo wanatakiwa kuwafundisha tabia njema, uzalendo na nidhamu ili kujenga taifa la watu waadilifu wanaoipenda nchi yao.

 

Hata hivyo, alieleza kuwa jukumu la malezi kwa watoto haliwezi kusimamiwa na mwalimu peke yake bali wazazi/walezi, viongozi wa siasa na dini na jamii kwa ujumla  wana wajibu kushirikiana na kumsaidia mwalimu  ili kusaidia watoto kukua katika maadili mema yanayozingatia utamaduni wa kitanzania.

 

Katika ziara hiyo, Dkt. Msonde aliambatana na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Prof. Willy Komba, Katibu wa TSC, Mwl. Paulina Nkwama, Katibu Tawala Msaidizi (Elimu) wa Mkoa wa Morogoro, Germana Mung’aho pamoja na watendaji wengine wa TSC ambao wapo mkoani Morogoro kwa ajili ya kikao ka