Mwl. Nkwama Awapongeza Walimu Wote Nchini Wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani

13 Oct, 2025
Mwl. Nkwama Awapongeza Walimu Wote Nchini Wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani

Katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani tarehe 5 Oktoba 2025, Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu alitumia fursa hiyo kuwatakia walimu wote nchini na duniani heri ya maadhimisho, akisisitiza mchango wao mkubwa katika malezi, mafunzo na ujenzi wa kizazi chenye maarifa, maadili na uzalendo.

Akizungumza kwenye sherehe zilizofanyika Viwanja vya Kilimani, Katibu wa Tume alibainisha kaulimbiu ya mwaka huu ya kimataifa, “Recasting teaching as a collaborative profession”, ikisisitiza umuhimu wa taaluma ya ualimu kama kazi ya ushirikiano.

Aidha, akizingatia uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 29 Oktoba 2025, alihimiza walimu kushiriki kikamilifu kuchagua viongozi bora watakaoleta maendeleo ya kweli katika sekta ya elimu.

Mwl. Nkwama alisisitiza kuwa Tume ya Utumishi wa Walimu inaendelea kushirikiana na walimu kuhakikisha haki zao za kiutumishi zinadumishwa, mazingira ya kazi yanaboreshwa, na maadili ya taaluma yanazingatiwa.