TSC KUTEKELEZA VIPAUMBELE SITA VYA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA UJAO WA FEDHA WA 2024/25

19 Apr, 2024
TSC KUTEKELEZA VIPAUMBELE SITA VYA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA UJAO WA FEDHA WA 2024/25

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Tume ya Utumishi wa Walimu inatarajia kutekeleza vipaumbele sita vya Mpango wa Bajeti ya mwaka ujao wa fedha wa 2024/25.

Ametoa kauli hiyo tarehe 16 Aprili, 2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa Mwaka wa Fedha 2024/25.

Mhe. Mchengerwa alisema Tume itasimamia ajira, maadili, nidhamu na maendeleo ya walimu kwa kuhakikisha walimu wanasajiliwa, wanathibitishwa kazini na kwa wale wenye sifa wanapandishwa vyeo na wanabadilishiwa vyeo kwa wakati.

Alisema eneo jingine ni kufanya utafiti na kutathmini hali ya walimu nchini na kuwezesha

 wa matumizi ya mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Mhe. Mchengerwa alisema TSC itaboresha utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu za walimu, kuwajengea uwezo watumishi wa Tume na kuwezesha mazingira bora ya kufanyia kazi.