Idadi ya Walimu 274,541
Kwa upande wa Tanzania walimu walioajiriwa katika utumishi wa umma wanaofundisha kwenye shule za Msingi na Sekondari Tanzania Bara wanahudumiwa na Tume ya Utumishi wa Walimu (Teachers’ Service Commission-TSC). Hadi kufikia mwezi Oktoba 2024, Tume inahudumia walimu 274,541 ambapo walimu 180,325 ni wa shule za Msingi na 94,216 ni wa shule za Sekondari.