Walimu Waliosajiliwa 6,963

Tume ya Utumishi wa Walimu inasajili walimu wanaofundisha Shule za Msingi na Sekondari mara baada ya kuajiriwa katika Utumishi wa Umma. Katika kipindi cha kuanzia mwezi Machi 2021 hadi Mwezi Machi 2022 jumla ya Walimu 6,963 walisajiliwa. Katika idadi hiyo, walimu 4,044 ni wa Shule za Msingi na walimu 2, 919 ni wa Shule za Sekondari.