Ujumbe wa Mwenyekiti

Ni heshima kubwa kuwakaribisha kwenye tovuti ya Tume ya Utumishi wa Walimu. Nina uhakika kuwa maudhui au taarifa zilizowekwa hapa ni za kuelimisha,  kuvutia na zinazoendana na matarajio yako kuhusu Tume ya Utumishi wa Walimu.

Tume ya Utumishi wa Walimu, Imekuwa ikitekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa chini ya Kifungu cha 5 cha Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu Na. 25 ya Mwaka 2015. Imepewa Mamlaka ya Kuajiri, Kupandisha cheo Walimu, Kuthibitisha kazini Walimu, na Kusajili Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari za Serikali.

Ili kudumisha  mawasiliano baina ya Tume ya Utumishi wa Walimu, Wadau na Umma kwa ujumla, tumedhamiria  kuhakikisha kuwa tovuti hii inapatikana muda wote  na kutoa taarifa halisi na kwa wakati.

Kupitia tovuti hii, ni matarajio yangu kuwa Wadau na Umma watapata uelewa kuhusu Dhima na Dira katika kuwahudumia walimu wa Shule za Msingi na Sekondari za Serikali Tanzania bara.

Karibu